Thursday, August 30, 2012
MWENYEKITI BMT AZINDUA ROCK CITY MARATHON 2012
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Dioniz Malinzi akikata utepe kuzindua tamasha la Rock City Marathon 2012, katika hafla iliofanyika jana katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Picha na Mwandishi wetu
Wadhamini wa tamasha la Rock City Marathon 2012, pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Dioniz Malinzi (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika jana katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
======= ====== ======
MWENYEKITI wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua toleo la nne mbio za Rock City Marathon, zitakazofanyika kuanzia Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Akizungumza katika uzinduzi huo jana kwenye hoteli ya New Africa, Dar es Salaam, Malinzi alisema ni wakati wa kukufua vipaji vya mchezo wa riadha nchini.
“Kwanza nawashukuru Kampuni ya Capital Plus Internationa kwa kuendelea kuandaa mbio hizi kwa miaka mine sasa, sio siri michezo Tanzania imedorora, kwani tumechukua dhamana ya michezo lakini baadhi ya watu wamekua walafi, wanajenga majumba Mbezi Beach na kuendesha magari ya kifahari.
“Hii yote imechangiwa na dhamana ya uongozi wa michezo kuwapa walafi ambao wametufikisha hapa, nawaomba Capital Plus International msiishie hapa, tunataka sasa tufufue vipaji vya riadha na mwaka huu tumeamua tuwe na mashindano ya Taifa ya Riadha,” alisema Malinzi.
Tukio hilo limewavutia wadau wengi michezo, pamoja na makampuni makubwa kama Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), African Barrick Gold, Nyanza Bottlers, Mfuko wa Pensions (PPF), Geita Gold Mine, TANAPA, Sahara Communication, ATCL, New Mwanza Hotel, Airtel, na New Africa Hotel ambao wamejitokeza kudhamini mbio hizo.
Alisema mbio za mwaka huu zitahusisha mashindano mbalimbali kama vile mbio za nyika kilomita 5, (ambazo sio za ushindani), bali zitafanyika kama moja ya maandalizi ya mbio za mfano wa Marathon (mini marathon), pia kutakuwa na mbio za nusu Marathon za kilomita 21, mbio za kujifurahisha maarufu kama Fun Race (Classic for all) kilomita 5, mbio za walemavu za kilomita 3, mbio za watu wazima za kilomita 3 na mbio za watoto kuanzia miaka saba hadi 10 zenye urefu wa kilomita 2.
Kwa upande wake Msemaji wa Capital Plus International, Dk. Ellen Otaru, alisema mbio hizo zinaenda sambamba na kuhamasisha Utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo, ambapo washiriki watakua ni kutoka Ziwa Victoria na nchi jirani kama Kenya, Uganda, Afrika Kusini na baadhi ya Mataifa ya Ulaya.
“Ningependa kutoa shukrani kwa wafadhili mbalimbali waliofanikisha mashindano haya, nasi Capital Plus International, tunataka kuwahakikishia kuwa tunakuza riadha nchini na kuleta medali za dhahabu,” alisema.
Kwa upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Riadha Tanzania (RT), William Kalage, alisema wameridhia uwezo wa Capital Plus International katika kuandaa mbio hizo kwa mara ya nne kwa ufanisi.
“Sote tunatambua mchezo wa riadha ndio ulioipa sifa nchi yetu, lakini kwa sasa imedorora, safari ya kuiletea medali nchi yetu imeanza na lazima tuwekeze kwenye riadha ili tupate medali,” alisema Kalage.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment